Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan yatoa dola milioni 10 kusaidia wakimbizi wa kipalestina Syria: UNRWA

Mwanamke anapokea msaada kutoka UNRWA. Picha: UNRWA

Japan yatoa dola milioni 10 kusaidia wakimbizi wa kipalestina Syria: UNRWA

Msaada wa Kibinadamu

Serikali ya Japan imetoa dola milioni 10 kusaidia shughuli za  kibinadamu za shirika la Umoja wa Mataifa la usaidizi kwa wakimbizi wa kipalestina UNRWA, ili kutoa usaidizi kwa wakimbizi wa kipalestina nchini Syria, Lebanon na Jordan.

Bwana Pierre Krähenbühl ambaye ni mkuu wa UNRWA anakaribisha msaada huo kutoka serikali ya Japan huku  akitoa wito kwa wahisani kuweza kusaidia shirika hilo ambalo linahitaji kiasi cha dola milioni 409 ili kuweza kusaidia shughuli za dharura za kibinadamu , na mahitaji  mbalimbali ya wakimbizi wa kipalestina  nchini Syria ambao  wengi wao ni wahitaji wakubwa wa misaada ya kibinadamu.

Aidha Bw. Krähenbühl amesema Japan ni moja ya wahisani wakubwa waliojitolea  kuisaidia UNRWA ambapo tangu mwaka 2017 mpaka sasa wametoa kiasi cha dola milioni 43.3 katika programu mbalimbali kwa wakimbizi wakipalestina.

Japan imeendelea kuwa moja  kati ya wahisani 7 wanaotoa msaada kwa UNRWA tangu mwaka 1973 ili kuwesha shughuli za wakimbizi wa kipalestina duniani kote.