Zaidi ya miaka 400 iliopita watu millioni 15 walipelekwa utumwani

27 Aprili 2018

Wanafunzi mbalimbali kutoka nchi tofauti duniani wameshirika katika mdahalo kupitia video kama sehemu  ya kuwaenzi wahanga  wa biashara ya utumwa hususan ile ya kuvuka bahari ya Atlantiki.

Mkutano huo wa video ulikuwa na kauli mbiu ya  kumbuka utumwa vita na ushindi kupigania uhuru na usawa na kitovu cha mdahalo huo kilikuwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani  ambapo miongoni mwa wanafunzi waliounganishwa moja kwa moja na mkutano wa New York kupitia video ni wanafunzi wa Mexico pamoja na Tanzania. Baadhi ya walioshiriki wanaeleza jinsi mdahalo ulivyokwenda akianza Hussein Hamis kutoka shule ya upili ya Azania.

(SAUTI ZA WANAFUNZI TZ)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika ujumbe wake kwa shereza kumbukumbu ya biashara ya watumwa amesema, biashara ya watumwa kuvuka bahari ya Atlantiki ilikuwa biashara haramu na moja wa tukio la kuwahamisha  binadamu kutoka bara moja hadi lingine. Ameongeza kuwa watu zaidi ya millioni 15, wake kwa waume pamoja na watoto kutoka Afrika  waliwekwa utumwani na wanaenziwa wale waliyotokomea katika biashara hiyo haramu ili kuweza kulinda kila mwanadamu.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter