Sheria za kimila za umiliki wa ardhi ni muarobaini- Dkt. Laltaika

27 Aprili 2018

Baada ya mashauriano na mazungumzo kwa wiki mbili, hatimaye mkutano wa 17 wa jukwaa la kudumu la watu wa asili la Umoja wa Mataifa unatamatisha shughuli zake jijini New  York, Marekani.

Jukwaa la kudumu la watu wa asili la Umoja wa Mataifa linakunja jamvi leo Ijumaa huku washiriki wakiweka msisitizo suala la kujumuisha sheria za umiliki wa ardhi za kimila ili kuepuka mizozo ya umiliki wa ardhi za watu wa jamii hiyo.

Akihojiwa na Idhaa ya UN kando ya jukwaa hilo, Dk Elifuraha Laltaika, ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa hilo amesema msisitizo huo unazingatia kwamba..

(Sauti ya Dkt. Elifuraha Laltaika)

Alipoulizwa iwapo sheria hizo si kandamizi hasa kwa jinsia ya kike kwenye umiliki wa ardhi, Dkt. Laltaika amesema..

(Sauti ya Dkt. Elifuraha Laltaika)

 Jukwaa hilo limefanyika kwa wiki mbili ambapo suala la ardhi ya watu wa jamii ya asili lilipatiwa kipaumbele kikubwa wakati huu ambapo baadhi ya shughuli za maendeleo zinawanyika haki yao ya msingi ya kuendelea kuishi kwenye maeneo yao ya asili.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter