Watoa misaada ni lazima walindwe. Guterres
Mfanya kazi mmoja wa kutoa misaada ya kibinadamu wa chama cha msalaba mwekundu na hilali nyekundu-ICRC ameuawa na watu wasiojulikana waliokuwa wamebeba silaha mjini Taizz nchini Yemen
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres , kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Stephane Dujarric , amelaani shambulio hilo na kutaka waliotekeleza kitendo hicho wakamatwe na kuchukuliwa hatua za sheria.
Amekariri kuwa pande zote husika katika mgogoro nchini Yemen ni sharti wawape ulinzi watoa misada ya kibinadamu kwa watu wa Yemen zaidi ya milioni mbili wanaohitaji msaada.
Taarifa za tukio hilo zinasema kuwa mfanya kazi huyo aliuawa katika viunga vya Taizz, wakati genge la watu wenye silaha lilipovamia gari la chama cha msalaba mwekundu.