UNFPA yajipanga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ifikapo 2030
Mkutano wa kikanda ulioandaliwa na shirika la afya ulimwenguni WHO huko Coimbra Ureno, umeyakutanisha mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na ya kibinadamu ili kujadili mikakati madhubuti kuhusu upatikanaji wa bima ya afya hususan kwa watu wasio na uwezo katika nchi masikini duniani.
Bi Monica Ferro ni mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA katika ofisi ya Geneva Uswisi ambaye kwenye mahojiano na idhaa wa Umoja wa Mataifa amesema amewakilisha shirika lake kwenye mkutando huo ili kujadili umuhimu wa kuwekeza katika afya ya mwanamke ikiwa ni njia ya kukabili matatizo ya kimaendeleo na ya kijamii .
Sauti ya Monica Ferro
Ni muhimu kuwekeza katika afya yao, ni muhimu kuwekeza katika upatikanaji wa uzazi wa mpango ili kuwapa fursa ya kupanga mwelekeo wa maisha ya baadaye katika kupata elimu ya kutosha ili kuwapa uwezo na ujasiri wa kuamua maisha yao ya baadaye na pia fursa ya ajira nzuri kama ilivyo kwenye mpango wetu wa kutomuacha mtu yeyote nyuma.
Na kuhusu mikakati itakayojadiliwa kwenye mkutano huo ili kufikia malengo ya mendeleo endelevu ya mwaka 2030 Bi Ferro amesema
Sauti ya Monica Ferro
Majadiliano yetu katika mkutano huu yanajikia katika vipengele vitatu ambavyo UNFPA imejiwekea ili kufikia 2030. Vipengele hivyo ni kutosheleza huduma ya afya ya uzazi , kusiwepo na vifo wakati wa kujifungua, na kusiwepo na vitendo vya aina yeyote vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwa ni pamoja na ukeketaji kwa wasichana.