Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati umewadia maazimio katika karatasi kuwa vitendo mashinani: UN

Picha: UM/Albert González Farran
Wanawake wanaokumbwa na ubakaji husalia na msongo.

Wakati umewadia maazimio katika karatasi kuwa vitendo mashinani: UN

Haki za binadamu

Ukatili wa kingono katika maeneo ya vita na machafuko umebainika kuwa moja ya sababu kubwa za watu kutawanywa.

aHayo yamejitokeza katika mjadala wa wazi uliofanyika leo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani ukijikita katika ukatili wa kingono katika mizozo na nini kifanyike kukomesh chini ya mada wanawake, amani na usalama..

Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed akihutubia Baraza la Usalama katika mjadala kuhusu wanawake, amani na usalama.
UN Photo/Mark Garten)
Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed akihutubia Baraza la Usalama katika mjadala kuhusu wanawake, amani na usalama.

Akuzungumza katika ufunguzi wa mjadala huo naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Amina . J. Mohammed na kutolea mfano madhila yanayoisibu jamii ya Rohingya amesema

(SAUTI YA AMINA J MOHAMMED)

“Mwaka huu , nchini Myanmar na kwingineko kwenye vita, kusambaa kwa tishio na matumizi ya ukatili wa kingono kwa mara nyingine kumetumika kama mbinu za kutekeleza azma za kijeshi, kiuchumi na kijamii, na umekuwa ni chachu ya watu wengi kulazimika kutawanywa.”

Image
Hatua kuchukuliwa ili kukomesha ukatili dhidi ya wanawake. Picha:UN Women/Daniel Hogson

Ameongeza kuwa ingawa waathirika wakubwa katika jinamizi hilo ni wanawake lakini

(SAUTI YA AMINA J MOHAMMED)

“ Wacha niseme bayana kwamba jinsia zote zinaathirika na ukatili huu wa kingono katika vita, na ukatili huo mara nyingi hutumika pia kama njia ya kuwatesa mahabusu, na katika mizozo mahabusu walio wengi ni wanaume na wavulana, lakini kwa ujumla wanawake na wasicha ndio waathirika wakubwa.”
Naye mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo Pramila Patten katika mjadala huo amesisitiza kuwa wakati umefika kugeuza maneno na maazimio yaliyomo katika karatasi kuzaa matunda mashinani kwani

Pramila Patten, Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo akifungua kikao cha Baraza la Usalama kuhusu wanawake, amani na ulinzi wa amani.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Pramila Patten, Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo akifungua kikao cha Baraza la Usalama kuhusu wanawake, amani na ulinzi wa amani.

(SAUTI YA PRAMILA PATTEN)
 “Wakati kumekuwa na hatua kubwa katika masuala ya operesheni, lakini ni dhahiri shairi kwamba maneno yaliyoko kwenye karatasi hayaoani na hali halisi mashinani, hatujaondoka kwenye maazimio na kuingia kwenye suluhu ya kudumu. Naamini tuko njia panda kwenye suala hili na ni lazima tupige hatua haraka kwa kuhakikisha uwajibikaji au tuko hatarini kubadili mwelekeo ambao utasababisha ubakaji katika vita kuwa tena jambo la kawaida kutokana na kiwango na ukwepaji wa sheria unaotendeka.”

Mjadala huo pia umehudhuriwa na bi Razia Sultana, mwanamke kutoka jamii ya Rohinya aliyesimulia hali halisi ya madhila yanayowakabili wanawake na wasichana wa jamii hiyo ambao hulengwa kwa makusudi  kwa sababu tu ya dini na kabila lao.