Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mimba za utotoni ni zahma kwa wasichana na jamii

Ndoa za utotoni zinazababisha wasichana kuacha shule
Photo: IRIN/Mujahid Safodien
Ndoa za utotoni zinazababisha wasichana kuacha shule

Mimba za utotoni ni zahma kwa wasichana na jamii

Wanawake

Mimba za utotoni ni changamoto kubwa nchini Tanzania na hususani katika maeneo ya vijijini.  Serikali ya nchi hiyo ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, ustawi wa jamii na mashirika ya kitaifa na kimataifa kama la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wanaelimisha jamii wakiwemo wasichana wadogo mashuleni athari za mimba hizo. 

Pelosi alikuwa na ndoto za kuwa mhadisi au daktari siku moja lakini sasa ndoto zake zimeishia kulea mtoto baada ya kupata ujauzito akiwa kidato cha pili kwenye shule ya sekondari ya Dumila mkoani Morogoro nchini Tanzania.

Akijutia kilichomsibu anaeleza sababu za tupa jalalani ndoto zake

(SAUTI PELOSI PAUL REUBEN)

Na je baba wa Pelosi alialichukua hatua gani baada ya tarifa hizo za masikitiko?

(SAUTI YA PAUL MPINA)

Pelosi ni kama tone la maji baharini ukilinganisha na idadi ya wasichana wanaokatiza masomo kutokana na mimba za utotoni.

Kwa mujibu wa takwimu za afisa elimu mkoani Morogoro, waathirika wakubwa ni wanafunzi wa shule za msingi kati ya umri wa miaka 13-15 , lakini wengi zaidi ni wa sekondari kati ya miaka 16-18 ambapo kuanzia Julai hadi Septemba 2017 watoto 301 walikatiza masomo kutokana na mimba za utotoni na hatua madhubuti zisipochukuliwa basi kutakuwa na mtihani mgumu wa kutimiza lengo la maendeleo endelevu nambari 4 la elimu bora likijuisha wasichana na wavulana ifikapo 2030.