Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya miaka 38 ya ndoa si kifo bali vita vyawatenganisha wanandoa

Hapa Koula, jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo watot waliorereja makwao wakiwa nje wakifuatilia darasa. Mzozo wa kivita jimboni humo umesabababisha wakazi wake kukimbilia na kusaka hifadhi kwingineko.
OCHA/Naomi Frerotte
Hapa Koula, jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo watot waliorereja makwao wakiwa nje wakifuatilia darasa. Mzozo wa kivita jimboni humo umesabababisha wakazi wake kukimbilia na kusaka hifadhi kwingineko.

Baada ya miaka 38 ya ndoa si kifo bali vita vyawatenganisha wanandoa

Amani na Usalama

Pater Juma Maru na Cecilia Ofowa ni wanandoa kwa miaka 38, raia hawa wa Sudan Kusini hivi sasa ni wakimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ingawa wanaonana , lakini hawawezi kuishi pamoja kama mke na mume kulikoni?

Wanandoa hao Peter na Cecilia kama walivyo maelfu ya raia wengine wa Sudan Kusini walilazimika kufungasha virago vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipochachamaa na kukimbilia DRC kusaka hifadhi.

Licha ya kuhepa kutenganishwa na kifo wakati wa vita nchini mwao, lakini sasa wamelazimika kutengana na kuishi tofauti kwa mara ya kwanza kabisa, kisa? uhaba wa malazi kwenye kambi za wakimbizi DRC.

(SAUTI YA PETER JUMA MARU)

“Mke wangu nakadiria anaishi kilometa mbili kutoka mahali ninapoishi, inanichukua muda kwenda, lakini namtembelea ingawa sio kila mara, namkumbuka sana, tumekuwa pamoja karibu maisha yetu yote sasa, tunazeeka pamoja.”

Naye Bi Cecilia Ofowa akiwa kwenye kambi ya wakimbizi inayohifadhi wanawake na watoto tu DRC, hakuficha hisia zake

(SAUTI YA CECILIA OFOWA)

“Inaumiza sana, sasa hivi sie ni wazee, nataka aje hapa ili tuishi pamoja na wajukuu zetu na hata watoto wetu hadi pale Mungu atakaponitenganisha naye.”

Peter amekuwa akiishi kwenye kibanda kidogo cha nyasi kwa miezi minane na hali si shwari hata kidogo

(SAUTI YA PETER JUMA MARU)

“Upepo uvumapo unanifikia, wakati mvua ikinyesha inaingia ndani, Ni hali mbaya, ni mazingira magumu. Nahisi kwa kiasi kikubwa kutokuwa na matumaini kabisa”

Peter anatumia siku nyingi kujikumbusha ya kale akiwa na hamasa kubwa ya kutaka kurejea nyumbani kwakwe na kwa mkewe, lakini kama walivyonena wahenga , ya kale si dhahabu tena.