Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani mashambulizi dhidi ya walinda amani Mali.

Helmeti za Buluu na sare za askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Picha:Umoja wa Mataifa Picha / Marco Dormino

Guterres alaani mashambulizi dhidi ya walinda amani Mali.

Amani na Usalama

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulizi  dhidi ya askari walinda amani wa Umoja wa Mataifa  huko Timbuktu Mali April 14, ambapo askari mmoja kutoka Burkina Faso alipoteza maisha,  wengine7 kutoka Ufaransa na  raia 2 kutoka Mali kujeruhiwa.

 

Bwana Guterres kupitia msemaji wake, ametuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Burkina Faso na pia familia ya marehemu, huku akiwatakia ahweni  askari majeruhi katika shambulizi hilo na  walinda amani wote wanaojitolea usiku na mchana kwa lengo la kutoa ulinzi kwa mamilioni ya raia duniani kote.


Aidha Bw. guterres ametoa wito kwa serikali ya Mali na makundi ya wanamgambo waliosaini mkataba wa amani kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika, na kuwachukulia hatua za kisheria haraka iwezekano.

Pia amesema, vitendo hivyo vya kikatilidhidi ya asakari walinda amani havitarudisha  mchakato wa amani unaofanywa na MINUSMA na kila shambulizi dhidi ya walinda amani, ni ukiukwaji wa sheria za kivita na  za kimataifa, hivyo atakaekutwa na hatia  atachukuliwa hatua kali.