Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN na AU walaani vikali mauaji ya walinda amani CAR

Kikosi cha Burundi kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA. Picha ya MINUSCA.

UN na AU walaani vikali mauaji ya walinda amani CAR

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika (AU)  kwa pamoja wamelaani vikali mauaji ya walinda amani wawili wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA ambapo walinda amani wengine wanane wamejeruhiwa.

Taarifa ya pamoja ya  iliyotolewa leo na mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix na  kamishina wa masuala ya amani na usalama wa AU Smail Chergui ambao wameanza ziara ya siku nchi nchini CAR , inasema mauaji hayo ya mlinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA,  yalitokea wakati wa majibizano ya risasi na watu wenye silaha wanaohusiana na kundi la Anti-Balaka mjini Bangui.

Akishikamana na serikali ya Rwanda, familia za walinda amani waliouawa na waliojeruhiwa Chergui amesema

(Sauti ya Smail Chergui)

“Bila shaka tulikuwa na fura ya kipekee leo asubuhi kupokelewa na Waziri Mkuu, mimi na mwenzangu Jean-Pierre Lacroix na ilikuwa ni fursa ya kuwambuka na kutoa pole kwa askari wetu wawili waliouawa jana wakiwa katika harakati za kulinda Amani na utulivu Jamhuri ya Afrika ya Kati.”

Kwa upande wake Lacroix akisisitiza kwamba mashambulizi hayo hayatereshi mshikamano wa Umoja wa Mataifa na AU ameongeza

(Sauti ya Jean-Pierre Lacroix)

“Kilicho muhimu ni kuonyesha umoja kati ya mashirika yetu na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusongesha jitihada za kisiasa na azma ya Afrika ya mashariano ya amani na kuunga mkono jitihada za MINUSCA za kulinda raia bila kusahau kuimarisha uchumi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. « 

Shambulio hilo limefuatia operesheni ya pamoja iliyozinduliwa Aprili 8 baina ya MINUSCA vikosi vya CAR vikijumuisha polisi ya kuwapokonya silaha na kuwakamata makundi ya wahalifu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameongza sauati yake katika kulaani shambulio hilo akitaka uchunguzi wa kina ufanyike na kukumbusha kuwa mashambulizi dhidi ya walinda amani yanaweza kuwa ni uhalifu wa kvita.