Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliofariki dunia Douma wakutwa na dalili za kuvuta hewa kali ya sumu- WHO

Moja ya mitaa huko Douma, eneo la Ghouta mashariki nchini Syria ambako mapigano yamesambaratisha maeneo ya makazi.
UNICEF/Amer Al Shami
Moja ya mitaa huko Douma, eneo la Ghouta mashariki nchini Syria ambako mapigano yamesambaratisha maeneo ya makazi.

Waliofariki dunia Douma wakutwa na dalili za kuvuta hewa kali ya sumu- WHO

Amani na Usalama

Watu 43 waliofariki dunia huko Douma, Syria baada ya shambulio la jumamosi wameripotiwa kuwa na dalili za kuvuta hewa kali yenye kemikali ya sumu.

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema idadi hiyo ni miongoni mwa watu 70 waliofariki dunia baada ya kushambuliwa wakiwa wamejificha kwenye mahandaki.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO anayehusika na masuala ya dharura Dkt. Peter Salama vifo hivyo ni miongoni mwa wagonjwa 500 waliosaka huduma huko Douma wamenukuu wadau wao wa afya wakieleza kuwa mifumo ya kupumua ya wagonjwa hao ilikuwa imeharibika sambamba na mfumo wa fahamu.

Halikadhalika wakati wa shambulio hilo vituo viwili vya afya vilishambuliwa.

Dkt. Salama amesema pamoja na kuchukizwa na shambulio hilo wanachotaka sasa ni wapatiwe fursa ya kuweza kufika ili waweze kutathmini kiwango cha athari za kiafya za shambulio hilo pamoja na kusaidia wahitaji.

Kwa sasa WHO inaratibiana na wadau wake wa afya ili kusaidia wakimbizi wa ndani huko Ghouta Mashariki nchini Syria sambamba na kuwasilisha misaada pindi watakapopata fursa ya kufanya hivyo.

Hapo jana, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishindwa kupitisha maazimio matatu yaliyolenga kwa njia moja au nyingine kuwezesha uchunguzi dhidi ya shambulio linalodaiwa kuwa la silaha za kemikali huko Douma.