Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya safari za kukata tamaa kupungua, hatari ipo palepale :UNHCR

Mkimbizi mwanamke kutoka Eritrea akiwa na rafiki wake katika basi ya kusafiririsha wakimbizi kutoka Libya kuelekea Ulaya.
UNHCR/Alessandro Penso
Mkimbizi mwanamke kutoka Eritrea akiwa na rafiki wake katika basi ya kusafiririsha wakimbizi kutoka Libya kuelekea Ulaya.

Licha ya safari za kukata tamaa kupungua, hatari ipo palepale :UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Licha ya kupungua kwa idadi ya wakimbizi na wahamiaji wanaokwenda kusaka hifadhi Ulaya , hatari zinazowakabili njiani watu hao kwa kiasi fulani zimeongezeka, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. 

Ripoti hiyo iliyopewa jina “Safari za kukata tamaa” inaonyesha mabadiliko ya mwenendo wa safari za wakimbizi na wahamiaji kuingia Ulaya, na inasema mwaka jana 2017, watu wapya waliowasili Italia wengi kutoka Libya , imepungua kwa kiasi kikubwa na imeendelea kupungua katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu 2018 ambapo idadi imeshuka kwa asilimia 74 ikilinganishwa na mwaka jana.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa pamoja na kupungua idadi ya waendao Ulaya safari ya Italia imethibitika kuwa yenye hatari zaidi na, kiwango cha vifo kati ya wale wanaovuka kutoka Libya iliongezeka hadi mtu 1 kwa kila watu 14 katika miezi mitatu ya kwanza ya 2018, ikilinganishwa na mtu 1 kwa kila watu 29 katika kipindi kama hicho mwaka 2017.

Pia ripoti imeaninisha madhila wanayopitia wahamiaji na wakimbizi wanaoomba hifadhi hususani wanawake na watoto  licha ya kupoteza maisha yao ikiwemo ukatili wa kingono na mateso kutokana na ulafi wa wasafirishaji haramu, magenge ya wahalifu na makundi yenye .

Na kufuatia sheria Kali za kuwabana wakimbizi na wahamiaji katika baadhi ya nchi za Ulaya ripoti inasema waomba hifadhi pia wamebadili mwelekeo na kutafuta njia mbadala za kufika Ulaya mfano kupitia Hispania ambako 2017 kumeshuhudiwa ongezeko la asilimia 101 la waomba hifadhi ikilinganishwa na mwaka 2016.