Kinachoendelea Gaza unawezakuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu: ICC

9 Aprili 2018

Ghasia dhidi ya raia na hali kama inayoendelea Gaza hivi sasa inaweza kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu chini ya mkataba wa Roma wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu au ICC, hasa kwa kutumia uwepo wa raia kama ngao kwa operesheni za kijeshi.

Onyo hilo limetolewa leo na mwendesha mashitaka mkuu wa ICC, Bi Fatou  Bensouda akisisitiza kuwa mahakama hiyo inafuatilia kwa karibu na hofu kubwa ghasia na kuendelea kuzorota kwa hali kwenye Ukanda wa Gaza kufuatia maandamano makubwa ya hivi karibuni.

Tangu tarehe 30 Machi 2018 takriban Wapalestina 27 wameripotiwa kuuawa na vikosi vya ulinzi vya Israel na wengine zaidi ya 1000 kujeruhiwa , wengi wao kutokana na kupigwa na risasi za moto na risasi za mpira.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter