Huduma ya afya kwa wote ni zaidi ya kuwa na bima: WHO

6 Aprili 2018

Huduma ya afya kwa wote ambayo ni kauli mbiu ya siku ya afya duniani mwaka huu ni zaidi ya kuwa na bima ya afya limesema shirika la afya ulimwenguni WHO. 

Shirika hilo limesema kuna baadhi ya nchi zimepiga hatua kubwa katika kuelekea utimizaji wa lengo la afya kwa wote kwa kuzingatia ajenda ya maendeleo endelevu au SDGs ya mwaka 2030, lakini bado nusu ya watu wote duniani hawawezi kumudu kupata huduma za afya wanazohitaji.

Katika ujumbe wake wa siku ya afya duniani itakayoadhimishwa kesho Aprili 7, mkurugenzi mkuu wa WHO Dr. Tedros Gabreyesus amesema endapo nchi zitataka kutimiza lengo la afya hapo 2030 basi itabidi watu bilioni moja wafaidike na huduma ya afya kwa wote (UHC) ifikapo mwaka 2023, lasivyo lengo hilo halitotimia.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu anayestahili kuchagua kati ya kununua dawa au kununua chakula, naye Dr. Hillary Kipruto wa WHO nchini Kenya amekumbusha kwamba huduma kwa wote si kitu kimoja

(SAUTI YA DR HILLARY KIPRUTO)

Na hivyo ameshauri

(SAUTI YA DR HILLARY KIPRUTO)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter