Polisi wanapomwepusha msichana na FGM

5 Aprili 2018

Ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake unasalia kuwa ni jambo linalotishia tu siyo afya ya kundi hili bali pia maendeleo yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Sasa watoto wenyewe wa kike wanasimama kidete kuhakikisha hawakumbwi na kikwazo hicho.

Harakati za kuondokana na ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake , FGM, zinazaa matunda pale msichana anapopaza sauti na jamii yake kuitikia.

Hiyo imekuwa dhahiri kwa Purity Soinato Oiyie, msichana wa kimasai kutoka Kenya ambaye akiwa na umri wa miaka 11 alikwepa kitendo hicho haramu.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Purity amesimulia alifanikiwa vipi kukwepa mkono wa ngariba.

(Sauti ya Purity Soinato Oiyie)

Hivi sasa Purity mwenye umri wa miaka 22 amefanikiwa kuhitimu shahada yake ya kwanza ya Chuo Kikuu akijikita katika masuala ya elimu. Pamoja na kwamba ni mjumbe wa Bodi ya kitaifa nchini Kenya ya kukabiliana na FGM, Purity hutumia muda wake mwingi kuhamasisha wasichana na jamii dhidi ya , ukeketaji. Je mwitiki uko vipi?

(Sauti ya Purity Soinato Oiyie)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter