Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia kwaheri kwa sasa:UN

Walinda amani nchini Liberia. Picha ya UNMIL/Staton Winter

Liberia kwaheri kwa sasa:UN

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Liberia UNMIL leo umefunga rasmi mlango ulioufunguliwa miaka 15 iliyopita.

Kupitiataarifa iliyotolewa na msemaji wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha mafanikio ya kufungwa rasmi leo 30 Machi 2018 kwa mpango huo.

Antonio Guterres amewapongeza watu na serikali ya Liberia kwa dhamira yao ya kugeuza ukurasa wa machafuko na vita kuwa amani. Pia ameipongeza serikali ya nchi hiyo kwa kuendelea na juhudi za kuhakikisha kunakuwa na amani na maendeleo endelevu Liberia.

Kamanda wa kwanza mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL Luteni Jenerali mstaafu Daniel  Ishmael Opande akiwa katika moja ya operesheni za Umoja wa Mataifa mjini Monrovia.
Picha na UN
Kamanda wa kwanza mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL Luteni Jenerali mstaafu Daniel Ishmael Opande akiwa katika moja ya operesheni za Umoja wa Mataifa mjini Monrovia.

Kwa upande wa UNMIL Katibu mkuu ameshukuru mchango mkubwa uliotoa kwa ushirikiano na wadau wengine hususani jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS ambayo walinda amani wake waliweka msingi wa mpango wa UNMIL kuingia na kusaidia mchakato mzima wa amani Liberia.

Guterres ameshukuru na kupongeza kazi nzuri iliyofanywa na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, wa sasa na waliotangulia,  wafanyakazi wasio askari na raia waliofanya kazi na UNMIL.

Image
Mlinda amani mwanamke wa UNMIL.(Picha:UM/Christopher Herwig)

Pia amewaenzi walinda amani 202 waliopoteza maisha yao wakati wa mika karibu 15 ya kazi ya UNMIL Liberia. Vikosi vyote vya jeshi na polisi amevipongeza kwa mchango mkubwa waliotoa na hususan nchi zilizochangia vikosi hivyo.

Image
Rais mteule wa Liberia, George Weah (kushoto) akizungumza na mmoja wa wageni kwenye hafla iliyoandaliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL baada ya kutangazwa rasmi kwa matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi nchini Liberia. (Picha:UNMIL Video capture)

Guterres meihakikishia Liberia kwamba Umoja wa Mataifa na familia yake utaendelea kuisaidia serikali ya nchi hiyo katika utekelezaji wa mipango ya mabadiliko ili kuhakikisha amani iliyopatikana kwa kazi ngumu inadumu na nchi hiyo na watu wake wanasonga mbele kimaendeleo.