Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvuvi wafufua matumaini ya wakimbizi Mediterania:UNHCR

Wavuvi wakiwa kazini Evia, Ugiriki
Picha ya UN Photo/Tsagris
Wavuvi wakiwa kazini Evia, Ugiriki

Uvuvi wafufua matumaini ya wakimbizi Mediterania:UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Huko Mediterania, wakimbizi wawili kutoka Mashariki ya kati, Syria na Iraq wamejenga urafiki usiotarajiwa kupitia ndoano ya uvuvi ambayo hawakuwahi kuitumia hata siku moja maishani . Ilikuwaje,?

Nats: sea waves

VOICE: Mawimbi yakivuma katika bahari ya Mediterania na kuruhusu Boti zilizosheheni mizigo, samaki n ahata wahamiaji na wakimbizi

 Nats

(SAUTI YA WALID) 

“Uvuvi umetufundisha kuwa wavumilivu, kuwa wanaotafakari na pia kutufanya kuwa pamoja kama marafiki”.

Hiyo ni sauti ya Walid Jaafar  mwenye umri wa miaka 37 mkimbizi kutoka Iraq akizungumza ufukweni mwa bahari katika kisiwa cha Crete katika bahari ya Mediterani.

Anasema uvuvi umewafunza mengi. Walid alikuwa mwalimu wa Fizikia mjini Baghdad  na alikuwa hana ujuzi wowote wa kuvua samaki.

(SAUTI YA ISMAIN)

“Nilikuja kuona maji ya baharí na kushudia wavuvi wa Kigiriki wakifanya kazi yao. Nilianza kuwatizama jinsi wafanyavyofanya kazi zao nami nikiwaiga.”

Huyo huyo ni Ismain Khalife mkimbizi kutoka Syria, mwenye umri wa miaka 50 akiwa na familia yake ya watu 13. Alijaribu mara 33 kuvuka  baharí kutoka Uturuki hadi Ugiriki lakini mambo yakagoma.

Wamekutana kwenye ufukwe wa baharí na tangu hapo wamekuwa marafiki. Jaffer asema urafiki wao umewasaidia sana.

(SAUTI YA WALID) 

“Tumesaidiana na tumejifunza. Tulianza kukutana kila siku”

 Wote wanapata msaada kutoka shirika la kuwahudumia wakimbizi laUmoja wa MataifaUNHCR kwa kuwapa makazi ya muda wakitafuta njia za kwenda kwengine kupitia majini. Je Walid jaffer haoni kama kuna hatari ya kutumia maji kuendelea anako taka yaani Ujerumani?

(SAUTI YA WALID) 

“Syria ilikuwa hatari mno kuliko kuvuka baharí “

Ismain na familia yake  wanasubiri kuunganishwa na mtoto wao aliyeko Ujeruamni ilhali Walid yeye anataka kubakli katika kisiwa hicho cha Crete kwa kuomba hifadhi..Kwa sasa wawilihao hupenda kwenda kwenye ufukwe na kukaa huko, kulikoni, anaeleza Ismail kutoka Syria.

( SAUTI YA ISMAIN )

Nats; sea waves

“Baharí inanipa amani rohoni kwani inanifanya nisahau matatizo yangu. Nataabika na msongo wa mawazo kutokana na mashambulizi pamoja na madhila tuliyopitia.”

 Walid pia ameneemeka na baharí

(SAUTI YA WALID )

Baharí iliniokoa. Na inanipa faraja. Iliniokoa kuepuka kifo”.

Watu hawa wamepata urafiki wakiwa uhamishoni na pia wana ari ya kuona kilichoko mbele.

Nats: Sea waves