Hati ya utambulisho wa stadi kuokoa wakimbizi Ulaya

28 Machi 2018

Mataifa ya Ulaya yameweka mbinu mpya za kuwasaidia wakimbizi katika bara hilo ili waweze kupata fursa ikiwemo ajira.

Mpango ambao umefanyiwa majaribio  mwaka 2017 na awamu mpya kuzinduliwa leo mjini Athens Ugiriki, unalenga kutambua viwango vya elimu vya wakimbizi, kazi gani wanaweza kufanya na pia lugha wanazozungumza ili kuwarahisishia mambo endapo hawana nyaraka mahsusi za kuwatambulisha.

Mradi huo wa hati hizo za utambulisho wa stadi za wakimbizi unatekelezwa kwa ubia kati ya shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR pamoja na Baraza la Muungano wa Ulaya ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kukabiliana na wimbi la wakimbizi hasa kutoka Mashariki ya Kati na Afrika.

Akiunga mkono mpango huo mwakilishi wa UNHCR kwenye Muunganowa Ulaya Roland-Francois Weil, amesema ni mzuri na wa kuaminika ambao unaweza kutumiwa  na taasisi za elimu ya juu, waajiri na washika dau wengine kuweza kusaidia alionayo kujumuishwa katika jamii.

Mbali na UNHCR mpango huo unaungwa mkono na Ugiriki, Italia, Norway, Uingereza, halikadhalika Ufaransa, Canada, Ujerumani na Uholanzi.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter