Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu yapiga chenga watoto milioni 2 Yemen

Mlinzi  katika shule apita ndani ya jengo mjini Sanaa Yemen ambalo liliharibiwa katika shambulio dhidi ya jengo la karibu
UNICEF/Mahmoud
Mlinzi katika shule apita ndani ya jengo mjini Sanaa Yemen ambalo liliharibiwa katika shambulio dhidi ya jengo la karibu

Elimu yapiga chenga watoto milioni 2 Yemen

Amani na Usalama

Mustakhbali wa takribani kizazi kizima cha watoto nchini Yemen bado uko mashakani

Wazee hawa wanarekebisha baadhi ya majengo yaliyobomolewa katika vita hivyo na miongoni mwa majengo hayo ni shule.

(watoto shuleni)

Kwa kuwa majengo ya shule yamebomolewa, sasa ni mahema yanatumika kufundishia watoto..

Kutokana na uharibifu wa majengo ya shule shirika la kuwahudumia watoto duniani, UNICEF linasema kuwa watoto takriban nusu milioni hawasomi tangu mapigano yaanze Yemen mwaka 2015.

Na shirika  limepiga mahesabu leo kuwa na idadi ya watoto milioni mbili ndio  hawaendi shuleni.

Hali hii imemfanya mwakilishi wa UNICEF nchini Yemen,  Meritxell Relano, , kunukuliwa akisema kuwa karibu kizazi kizima cha watoto wa Yemen kinakabiliwa na mustakhbali usioeleweka kutokana na kutopata elimu.

Ameongeza kuwa hata na wale waliobaki shuleni hawapati kiwango cha elimu wanachopaswa kukipata.

Ripoti ya UNICEF ikipatiwa jina “Ikiwa siko shuleni” inasema kuwa shule zaidi ya 2,500 hazifanyi kazi tena ambapo theluthi mbili ya shule hizo zimeharibiwa vibaya  katika mashambulio.

Nazo shule karibu asilimia 27 zimefungwa na zingine asilimia 7 zinatumiwa kwa harakati za kijeshi ama makazi kwa watu waliopoteza nyumba zao.

Na hata kwa watoto wanaotaka kwenda shule, safari nazo ni ngumu na za kutisha..

 (watoto shuleni)

UNICEF inaomba kwa niaba ya watoto wa Yemen, pande zote husika kumaliza vita hivyo.