Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbali ya adha, ukosefu wa maji huchagiza pia migogoro- UNAMID 

Kariya Mohamed Abbakar, mwenye umri wa miaka 50 kutoka eneo la Jebl Saiye Darfur Kaskazini nchini Sudan akijaza maji kwenye dumu la maji katika kisima cha karibu na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk.
UNAMID/Albert González Farran
Kariya Mohamed Abbakar, mwenye umri wa miaka 50 kutoka eneo la Jebl Saiye Darfur Kaskazini nchini Sudan akijaza maji kwenye dumu la maji katika kisima cha karibu na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk.

Mbali ya adha, ukosefu wa maji huchagiza pia migogoro- UNAMID 

Msaada wa Kibinadamu

Bado maji yamesalia kuwa rasilimali adimu kwa wakazi wa Darfur nchini Sudan.

Hali ya upatikanaji wa rasilimali ya maji kwa maelfu ya wakazi wa jimboni Darfur nchini Sudan ni mtihani mkubwa unaochangia pia kuendelea kwa migogoro.

Hayo yamesemwa leo na Olatunji Ayeni, mkuu wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur, UNAMID anayehusika na idara ya ulinzi wa amaji na mazingira, akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa wimbi kubwa la watu wanaohama maeneo mengine na kuingia Darfur, na hali ya ukame vimezidisha adha ya kupata rasilimali hiyo muhimu.

(Sauti ya Olatunji Ayeni)

“Hali ya upatikanaji wa maji safi Darfur ni mbaya hasa kwa upande wa maji ya kunywa, ukiangalia kwa upande wa rasilimali, hili ni moja ya eneo lenye hali mbaya sana ya hewa duniani, halina vyanzo vya rasilimali ya maji, halina mito, hivyo bado ni changamoto.”

Na kuhusu ongezeko la watu na migogoro amesema

(Sauti ya Olatunji Ayeni)

“Ongezeko la idadi ya watu hivi karibuni imeongeza changamoto kubwa katika rasilimali ya maji ambayo tayari ilikuwa adimu na ni vigumu kuiongeza, wanawake na wasicha ambao wangepaswa kuwa shule wanatumia sehemu kubwa ya maisha yao kwenda mbali kusaka maji. Ukiangalia kiukweli ni kwamba kiasili maji yamebainika kuwa ni moja ya sabau zisizo za kisiasa zinazochochea migogoro."