Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utachomaje mishikaki kwenye gesi? Ahoji Eddo

Mfanyabiashara wa mkaa chini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Matumizi fanisi ya mkaa yanaweza kusaidia kupunguza madhara ya tabianchi.
FAO/Giulio Napolitano
Mfanyabiashara wa mkaa chini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Matumizi fanisi ya mkaa yanaweza kusaidia kupunguza madhara ya tabianchi.

Utachomaje mishikaki kwenye gesi? Ahoji Eddo

Tabianchi na mazingira

Kila uchao Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake unapigia chepuo matumizi ya nishati mbadala kama njia mojawapo ya kuhifadhi misitu na hivyo kuepusha madhara zaidi yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO nchini Tanzania linaendelea na harakati zake za kusaidia serikali kuwa na sera bora za matumizi ya misitu na mazao yatokanayo na misitu hiyo.

Mwakilishi wa FAO nchini humo Fred Kafeero amesema hayo akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC nchini humo.

Bwana Kafeero amesema pamoja na harakati hizo kuna juhudi ambazo serikali inafanya..

(Sauti ya Fred Kafeero)

 “Inachukua muda kubadili watu kuacha kutumia kuni iwapo hakuna nishati mbadala. Na hapa Tanzania nadhani kuna juhudi kubwa za kufanya watu waache kutumia kuni na badala yake watumie gesi hususan maeneo ya mijini, jambo ambalo ni rasilimali muhimu ambayo nchi hii inayo hususan gesi asilia.”

Ili kufahamu changamoto za matumizi ya gesi ikilinganishwa na mkaa, Bi. Vuzo amezungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa kuchoma mishikaki eneo la Namanga, jijini Dar es saalam afahamikaye kwa jina la Eddo Chips ambaye amesema..

(Sauti ya Eddo Chips)