Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la uhamiaji si la mtu mmoja: UM

Jude Njomo, mbunge kutoka Kenya mwanachama wa IPU akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN
UN News/Patrick Newman
Jude Njomo, mbunge kutoka Kenya mwanachama wa IPU akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN

Suala la uhamiaji si la mtu mmoja: UM

Wahamiaji na Wakimbizi

Suala la uhamiaji sio la kushughulikiwa na mtu mmoja au taifa moja, linahitaji mshikamano wa kimataifa kulipatia ufumbuzi.

Hayo yamesemwa na William Lacy Swing, mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, akifungua mjadala wa kimataifa wa siku mbili mjini New York Marekani kuhusu ushirika bunifu na ujumuishwaji kwa ajili ya kushughilikia suala la kimataifa la uhamiaji na kutaja mambo matatu muhimu

(Sauti ya William Lacy swing)

Mosi majadiliano bado yanaendelea , na mkakati wenyewe unasisitiza umuhimu wa ushirika , pili tunahitaji kutoa msaada wa kiufundi , rasilimali na ushirika unaohitajika ili kushughulikia uhamiaji, na tatu tunayo ajenda ya 2030 inatotoa wito wa ujumuishwaji na ushirika wa uhamiaji.”

Na kuhusu suala la wafanyakazi wa nyumbani ambao pasi zao za kusafiri hukamatwa na waajiri, mbunge kutoka County ya Kiambu nchini  Kenya,  Jude Njomo alieshiriki mkutano wa wabunge kutoka chama cha wabunge duniani, mshiriki huyu alisema.

(Sauti ya Jude Njomo)

Mjadala huo umeyaleta pamoja mashirika na wadau mbalimbali  mkiwemo wakuu wa mashirika ya, UNICEF na ILO.