Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je redio za kijamii bado zina nafasi?

Wakazi wa Sangari Jamhuri ya Afrika ya kati wakisikiliza Radio Lego Tila Ouaka( Sauti ya Ouaka) redio ya jamii inawaleta pamoja waislamu na wakristo
Picha ya OCHA/Gemma Cortes
Wakazi wa Sangari Jamhuri ya Afrika ya kati wakisikiliza Radio Lego Tila Ouaka( Sauti ya Ouaka) redio ya jamii inawaleta pamoja waislamu na wakristo

Je redio za kijamii bado zina nafasi?

Wanawake

Redio za kijamii zina mchango mkubwa katika kumuendeleza mwanamke wa kijijini. Hiyo ni moja ya kauli zilizotanabaishwa wakati wa mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliomalizika hivi karibuni jijini New York, Marekani. 

Miongoni mwa washiriki ni Marceline Nyambala,  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la waandishi habari wa kike nchini Kenya ambaye ameelezea umuhimu wa redio za jamii wakati huu wa mitandao ya kijamii

(Sauti ya Marceline Nyambala)

Marceline Nyambala, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la waandishi habari wa kike nchini Kenya, AMWIK akihojiwa na UN News Kiswahili.
UN News/Selina Jerobon
Marceline Nyambala, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la waandishi habari wa kike nchini Kenya, AMWIK akihojiwa na UN News Kiswahili.

Katika mkutano huo washiriki walizungumzia pia changamoto ya redio hizo za jamii na jinsi ya kuzitafutia suluhisho kama anavyoelezea Nyambala.

 (Sauti ya Marceline Nyambala)