UN yalaani shambulio nchini Ufaransa.

24 Machi 2018

Umoja wa Mataifa unasimama bega kwa bega na serikali ya ufaransa katika vita dhidi ya ugaidi pamoja na misimamo mikali ya imani.

Kauli hiyo imetolewa leo  na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guteress, kupitia msemaji wake  Stéphane Dujarric kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya Ufaransa siku ya Ijumaa.

Katibu mkuu amevipongeza vikosi vya usalama vya Ufaransa kwa hatua ya haraka ambayo ilisaidia kuokoa maisha ya raia na pia kutoa pole kwa familia za wale walioathirika tukio hilo na wananchi na serikali ya Ufaransa.

Pia Katibu Mkuu amewatakia wale waliojeruhiwa wapate nafuu haraka.

Shambulio hilo la kigaidi lilitokea  katika mji wa Trebes ulioko kusini magharibi mwa Ufaransa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud