Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shaka yaondoka kwa watoto wenye TB Tanzania

Utoaji huduma kwa mgonjwa wa kifua kikuu.(Picha:UNifeed/video capture)

Shaka yaondoka kwa watoto wenye TB Tanzania

Afya

Sasa kila nchi inajizatiti kuondokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB ambao husababisha vifo vya watu 4500 kila siku kote duniani. Umoja wa Mataifa unasaka viongozi katika kila ngazi kuchukua hatua, nchini Tanzania serikali nayo imeonyesha njia ikiwemo kuimarisha ubia kati ya sekta ya umma na ile ya binafsi kwenye ugunduzi na upimaji wa TB.

Kuelekea siku ya kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, TB duniani hapo kesho, Tanzania imesema imeongeza idadi ya mashine za kisasa za kupima makohozi ya wahisiwa wa TB kutoka 66 mwaka 2015 hadi 186 mwezi huu wa Machi. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma hii leo ametaja sababu za kuanza kutumia mashine hizo ziitwazo GeneXpert badala ya X-Ray iliyozoeleka.

(Sauti ya Ummy Mwalimu)

Amesema mashine hizo zenye thamani ya shilingi milioni 38 kwa kila moja zimesambazwa pia katika hospitali binafsi na wameanzia na zile zilizoko mkoani Dar es salaam ambazo ni  Kairuki, Hindu Mandal, Agakhan, TMJ na Regency.

Waziri huyo wa afya pia ametangaza kuwa sasa Tanzania ina dawa ya kutibu TB kwa watoto, jambo ambalo amesema linamtia moyo zaidi ya kudhibiti ugonjwa huo miongoni mwa watoto.

(Sauti ya Ummy Mwalimu)