Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa natoka kijijini, ubunifu umeniokoa- Lydia

Lydia Jacob, mkulima na mjasiriamali kutoka Kisarawe Tanzania akiwa katika mkutano wa CSW62  makao makuu ya UN New York.
UN News/Patrick Newman
Lydia Jacob, mkulima na mjasiriamali kutoka Kisarawe Tanzania akiwa katika mkutano wa CSW62 makao makuu ya UN New York.

Ingawa natoka kijijini, ubunifu umeniokoa- Lydia

Wanawake

"Baada ya kupata mafunzo ya usindikaji bidhaa, nimeona mafanikio makubwa sana katika kilimo na biashara  na pia bidhaa zetu zinadumu muda mrefu bila kuharibika".

 

Hiyo ni kauli ya Lydia Jacob,  mkulima na mjasiriamali kutoka  Kisarawe, mkoa wa Pwani Tanzania.

Akihojiwa na Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa kando mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW62, jijini New York Marekani, Bi. Jacob amesema mafunzo ya usindikaji aliyopata yeye na wanawake wengine huko Kisarawe  yamewasaidia katika kukuza kilimo na biashara ya korosho.

(Sauti ya Lydia Jacob)

Na kuhusu mafanikio aliyoyapata kwa kushiriki kutano wa kamisheni ya hali wa wanawake na pia kupata fursa ya kuonyesha biashara yake ambayo sasa imevuka mipaka ya Tanzania, Bi. Jacob anasema.

(Sauti ya Lydia Jacob)