Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wana fursa ya kusaka suluhu ya wakimbizi:Model UN

Kundi la wanafunzi wanakihudhuria vikao vya Model UN kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
Picha na UN/DPI
Kundi la wanafunzi wanakihudhuria vikao vya Model UN kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa

Vijana wana fursa ya kusaka suluhu ya wakimbizi:Model UN

Wahamiaji na Wakimbizi

Vijana wana fursa klubwa ya kuchangia katika kupata suluhu ya changamoto za wakimbizi hususani barani afrika endapo watashirikishwa kikamilifu.

Maoni hayo yametolewa na baadhi ya vijana wanaoshiriki mfano wa vikao vya Umoja wa Mataifa (Model UN) mjini New York Marekani.

Wakizungumza na UN News wakati wakihitimisha hii leo vikao vya juma zima vijana hao kutoka chuo kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki kilichoko Nairobi Kenya wamesema vijana wakimbizi wana fursa ndogo sana ya kujiendeleza na hata ajira lakini kwa mawazo na nchango wa vijana wenzao wanaweza kupiga hatua.

 Emma Deraso Dokhole ni mmoja wa wanafunzi hao, ana asili ya Somalia na aliwahi kupitia kambi ya wakimbizi ya Daadab wakati wa utoto wake anasema

(SAUTI YA EMMA DERASO )

Kuhusu changamoto ya elimu kwa vijana hao wakimbizi Grace Njeri Ng’anga akaongeza

(SAUTI YA GRACE NJERI )