Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji katika mazingira ni tija kwa miji: FAO

icha hii ilipigwa Hanoi
Vietnam (Picha: UN/Kibae Park)
Mazingira ya mijini ni kero kwa wakazi iwapo usafi wake hautazingitiwa. P

Uwekezaji katika mazingira ni tija kwa miji: FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kuwekeza katika maeneo yenye mazingira bora ya kijani kunaweza kusaidia kubadili miji kuwa endelevu, yenye mnepo, yenye usawa na yenye kupendeza kuishi, limesema leo shirika la chakula na kilimo FAO likiadhimisha siku ya kimataifa ya misitu ambayo kila mwaka huwa Machi 21.

Shirika hilo linasema zaidi ya nusu ya watu wote duniani wanaishi mijini na ifikapo mwaka 2050 karibu asilimia 70 ya dunia itakuwa ni mjini. Ingawa miji inachukua asilimia tatu tú ya eneo la duniani lakini inatumua asilimia 78 ya nishati na kutoa asilimia 60 ya hewa ukaa.

Miji mingi kwa tayari imeonyesha jitihada zake za kutaka kuwa na mustakhbali endelevu,  na ni mifano mingi ya maendeleo ya miji yanayojali mazingira kwa mujibu wa ripoti ya FAO iliyochapishwa leo iitwayo “Misitu na miji endelevu-hadithi za kuhumiza kote duniani” ambayo pian dio kauli mbiu ya siku ya misitu mwaka huu.

Simone Borelli ni afisa misitu wa FAO anasema hali hiyo itakuwa na athari kubwa za kimazingira na kwamba

(SAUTI YA SIMONE BORELLI)

“Ukuaji huo kwa asilimia kubwa utakuwa haujapangwa, na wa kasi hususan maeneo kama Afrika na Asia na hivyo kuleta athari kubwa kwa mali asili zinazozungunga miji , na miji mingi itakabiliwa na changamoto kama umasikini, njaa , upungufu wa rasilimali, na itakabiliwa na athari za mmomonyoko wa mazingira kama mafuriko, upungufu wa maji, na maporomoko ya udongo.”

Ameongeza kuwa ingawa upanuzi huo wa miji utaathiri misitu lakini uhifadhi na upandaji wa miti mijini waweza kuwa dawa mjarabu

(SAUTI YA SIMONE BORELLI)

“Miti na misitu mijini inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuboresha uendelevu wa maendeleo ya miji na pia kuimarisha maisha ya jamii za mijini