Maji safi bado mkwamo kwa waRendile huko Marsabit

22 Machi 2018

Leo ni siku ya maji duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo uhifadhi wa mazingira halisi ya eneo husika kama njia moja ya kukabiliana na uhaba wa maji duniani.

Wavuti mahsusi wa siku hii  unatambua mabadiliko ya tabianchi pamoja na uchafuzi wa mazingira na shughuli za kibinadamu kuwa moja ya sababu za uhaba wa maji.

Hatua pendekezwa za kudhibiti ni pamoja na kuhifadhi maeneo asilia kwa kupanda miti na kuhifadhi maeneo oevu.

Huko kaunti ya Marsabit nchini Kenya, uhaba wa maji ni kikwazo kwa warendile ambao ni jamii ya wafugaji kama Alice Lesepen wa shirika la kiraia la KPL alivyoelezea akizungumza na idhaa hii.

(Sauti ya Alice Lesepen)

Hata hivyo kuna matumaini.

(Sauti ya Alice Lesepen)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud