Malengo ya SDG’s yatamalaki siku ya ushairi duniani

Picha:UNESCO

Malengo ya SDG’s yatamalaki siku ya ushairi duniani

Utamaduni na Elimu

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya ushairi duniani hii leo, siku iliyotengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO  kwa lengo la kuchagiza usomaji, uandishi, uchapishaji na ufundishaji wa ushairi, mwaka huu imetoa msukomo katika kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.

Tanzania haikusalia nyuma, kwa ushirikiano na kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC wamewashirikisha  washairi kuchagiza SDG’s , shairi la Love Mcharo ni miongoni mwa yaliyotawala, likighaniwa naye Nasir Ibrahim.