Wakimbizi wa Cameroon huko Nigeria taabani

20 Machi 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeshtushwa na ongezeko la idadi ya wakimbizi wa Cameroon  wanaosaka hifadhi Nigeria ambapo idadi yao sasa imefikia 20,000.

Aikaterini Kitidi ambaye ni msemaji wa UNHCR, mjini Geneva, Uswisi amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari  akisema kuwa taarifa kutoka kwa washirika wao ni kwamba zaidia ya asilimia 95 ya wasaka hifadhi wanakosa huduma muhimu kama chakula na malazi. 

Amesema baadhi ya familia wamebakiza mlo mmoja kwa siku moja kutokana upungufu wa chakula.

(Sauti ya Aikaterini Kitidi)

"Hadi sasa ofisi yetu imekuwa ikifanya  kazi ya kutoa huduma  kwa wakimbizi hawa chini ya mpango wa dharura wa dola 18 milioni. Hata hivyo, hadi sasa hakuna fedha zilizopokelewa, na kusababisha changamoto kubwa na mapungufu katika utoaji huduma."

Na kuhusu ushirikiano baina ya UNHCR na serikali ya Nigeria Bi Kitidi amesema

(Sauti ya Aikaterini Kitidi)

"Mapema mwezi huu, mamlaka nchini Nigeria ilitenga ardhi kwa UNHCR ambayo inapaswa kuruhusu makazi ya wakimbizi hao ili kuhakikisha usalama wao. UNHCR inaendelea kushirikiana mamlaka husika kususu kuhamishia makazi ya  wakimbizi angalau kilomita 50 kutoka mpakani, kulingana na sheria za kibinadamu."

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter