Bila takwimu mchango wa mwanamke kijijini hautojulikana:FAO

20 Machi 2018

Takwimu ni muhimu sana ili kuonyesha ni kwa kiasi gani mwanamke wa kijijini anachangia katika uzalishaji na maendeleo hasa katika vita vya ukombozi wake. 

Hayo yamesema na Bi Susan Kaaria afisa wa masuala ya jinsia idara ya será kwenye shirika la chakula na kilimo FAO. Akihojiwa na Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW, mjini New york Marekani, Bi Kaaria amesema wazalishaji wakubwa duniani ni wanawake hususani katika sekta ya kilimo, lakini thamani ya mchango wao haijulikani  kwa kuwa haijaorodheshwa popote

(SAUTI YA SUSAN)

Na amekumbusha kuwa bila wanawake wa vijijini hakuna maendeleo

(SAUTI YA SUSAN)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter