Rais wa Baraza kuu Miroslav ahitimisha ziara yake Colombia
Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Bwana Miroslav Lajčák, amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Colombia ambako alikutana na vyongozi wa ngazi ya juu serikalini na asasi za kiraia ili kuzungumzia azma ya utekelezaji wa amani na maendeleo andelevu SDGs.
Katika ziara yake Bw. Lajčák alikutana na rais wa Colombia Bw. Juan Manuel Santos Calderón ambapo wawili hao alizungumzia mchakato wa amani na ulinzi, ushirikiano baina ya Colombia na Umoja wa Mataifa, maendeleo ya kiuchumi kikanda, uhamiaji na malengo ya maendeleo endelevu ya kudumu (SDGs).
Aidha, Bw. Lajčák alimshukuru rais Santos kwa kukubali kuhudhuria mkutano wa ngazi ya juu kuhusu uimarishaji wa amani ya kudumu Colombia uliofanyika jijini Newyork mnamo tarehe 24 na 25 Aprili mwaka jana., na pia kwa ushirikiano wake na mkurugenzi wa mipango ya taifa Luis Fernando Mejía katika uzinduzi wa mkakati wa kitaifa Colombia wa kutekeleza SDGs.
Bwana Martín Santiago Herrero ambaye ni mwakilishi wa huduma za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Colombia amesema, ziara ya rais wa Baraza kuu nchini humo ni ishara ya ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Colombia katika uimarishaji na utekelezaji wa amani na maendeleo endelevu endelevu .