Wakimbizi wa DRC waendelea kumiminika Uganda: UNHCR

16 Machi 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR leo linasema  wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC- wanaoingia Uganda, wanaongezeka kila uchao kwa kiwango kisicho cha kawaida. 

UNHCR inasema wakimbizi hao ambao asilimia kubwa ni  wanawake na watoto wanatokea maeneo  ya Mashariki mwa DRC  . Kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR, Babar Baloch mbele ya waandishi habari mjini Geneva, Uswisi wakimbizi hao wanatoroka mapigano mabaya ya kikabila na pia vitendo vya unyanyasaji wa kingono vinavyoendelea nchini mwao.

(SAUTI YA BABAR)

“Katika kipindi cha siku tatu, kati ya tarehe 10 hadi 13 Machi, zaidi ya watu 4,000 walivuka mpaka na kuingia Uganda kutoka mikoa ya Ituiri,na Kivu kaskazini. Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na mwaka 2017 wakati takriban watu 44,000 walikimbilia machafuko kwa kipindi cha mwaka mzima.”

Ameongeza kuwa UNHCR inahofu kuwa huenda maelfu zaidi wanaweza kuwasili Uganda ikiwa hali ya kiusalama  ndani ya DRC haitotengamaa haraka.

Wakimbizi hao wanaoingia Uganda  kutoka Ituri wanatumia mitumbwi  ambayo ni hatari kwa usalama wao kuvuka ziwa Albert safari ambayo imesababisha baadhi ya wakimbizi kupoteza maisha yao.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter