Umiliki wa ardhi usiopokonyeka ni muarobaini wa ajenda 2030- LANDESA
Umiliki wa ardhi hasa miongoni mwa wanawake bado unasalia kukumbwa na utata hasa kwenye nchi ambako mila na desturi potofu zimeshamiri ili kuzuia umiliki huo. Sasa wanaharakati wanapigia chepuo umiliki kamilifu ambao kwao mwanamke au msichana ataendelea kumiliki ardhi hata anapokuwa hajaolewa, ameolewa au amesalia mjane.
Wanaharakati wa haki za ardhi kwa wanawake wametumia mkutanowa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW62 unaoendelea jijini New York, Marekani kutetea suala la umiliki usiopokonyeka.
Miongoni mwao ni Monica Mhoja, Mkurugenzi wa shirika la kiraia la utetezi wa haki ardhi kwa wanawake vijijini, LANDESA tawi la Tanzania ambaye akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili amesema mkutano huu..
(Sauti ya Monica Mhoja)
Amesema ni lazima ifahamike kuwa mwanamke anapokuwa na umiliki wa ardhi usiopokonyeka..
(Sauti ya Monica Mhoja)