Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji waendelea kuondoka Libya kwa hiari: IOM

Picha: IOM/Video capture
Alain, Mkimbizi mjasiriamali aliyejitolea kurudi nyumbani toka uhamiaji Libya.

Wahamiaji waendelea kuondoka Libya kwa hiari: IOM

Amani na Usalama

Juhudi za kuwasaidia wahamiaji kutoka Libya hadi nchi walikotoka  zasemekana  kuendelea vizuri umesema leo Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM Joel Millman hadi sasa shirika hilo limesaidi wahamiaji 10,171 kurejea kwao salama kutoka Libya kwa msaada  kutoka Umoja wa Ulaya, Muungano wa Afrika pamoja na serikali ya Libya.

Ameongeza kuwa idadi hiyo ya wahamiaji ni kuanzia Novemba 28 mwaka jana wakati operesheni  ya kurejea nyumbani kwa hiari -VHR ilipopewa msukumo.

 (SAUTI YA JOEL)

“Tunaendelea  kusaidia wahamiaji ambao wako ndani ya vituo wanamozuiliwa  nchini Libya huku juhudi zikiongezeka kuweza kuwafikia  wale wahamiaji waliokwama wakiwa nje ya vituo hivyo.”

 Ameongeza kuwa wahamiaji wengine 5,200 wamerejea nyumbani kwa msaada wa mataifa wanachama wa Muungano wa Afrika katika kipindi kimoja  hicho. Isitoshe amesema kuwa  wahamiaji wengine 23,302 wamerudi nyumbani kupitia mpango wa shirika la IOM wa kurejea kwa hiari-VHR tangu Januari mwaka 2017.

(SAUTI YA JOEL)

“Tangu kupanua opereshei za mpango wa VHR,idadi ya wahamiajai walioko katika vituo rasmi vya kuwahifadhi vimepungua  kutoka 20,000 mwezi wa Oktoba 2017 hadi 4,000 kufikia leo. Hii ikiwa ni upunguaji wa mara tano.”