Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mianzi na mabua vyageuzwa mlo Sudan Kusini

Wanawake huko Ganyiel jimbo la Unity nchini Sudan Kusini wakisubiri mgao wa chakula. Hali ni mbaya ya chakula.
OCHA/Gemma Connell
Wanawake huko Ganyiel jimbo la Unity nchini Sudan Kusini wakisubiri mgao wa chakula. Hali ni mbaya ya chakula.

Mianzi na mabua vyageuzwa mlo Sudan Kusini

Msaada wa Kibinadamu

Utapiamlo uliokithiri sasa ukumba tu siyo watu wazima bali pia watoto. Sasa wanaishi kwa kula mabua na mianzi porini.

Zaidi ya watu milioni saba nchini Sudan kusini sawa na theluthi mbili ya watu wote huenda wakakabiliwa na hali mbaya ya uhakika wa chakula katika miezi michache ijayo kusipopatikana misaada ya kibinadamu.

Onyo hilo limetolewa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo sasa linahaha kupata fedha za kutosha kutoa msaada kwa watu hao.

Hata Sudan Kusini mtoto Nyadane Kuony mwenye umri wa miaka minne akilia wakati anapimwa utapia mlo. Akiwa na babu na bibi yake  walikimbia vita huko Bentiu 2016, baba yake alifariki dunia kabla hajazaliwa na mama yake kwa sasa hayupo. Binti huyo alianza matatizo ya utapia mlo vita vilipochachamaa .

Hivi sasa kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula watu wamegeukia kula mianzi na matunda mwitu. Mine Pusk Luoch ana umri wa miaka 8 tu

(SAUTI YA MINE LUOCH)

"Nimekuja hapa kula mianzi hii kwasababu hatuna chakula.”

Maelfu ya wakimbizi wa Sudan kusini wanaendelea kumiminika katika nchi jirani ikiwemo Kenya ambako kambi ya Kakuma inahifadhi zaidi wakimbizi 106,000 kutoka sudan kusini. WFP inawapa msaada wa chakula wanapopokelewa tu kama anavyofafanua Martin Karimi msemaji wa shirika hilo nchini Kenya.

(SAUTI YA MARTIN KARIMI)

“Tunapokea takribani watu elfu moja kila mwezi, wanapowasili WFP inawapa mlo wa moto kabla hawajapewa vipande vya ardhi ambako wataendelea kupokea mgao wa chakula pamoja na fedha taslim kutoka WFP.”

Hivi sasa WFP inatoa chondechonde kwa wahisani na wafadhili kutoa fedha ili kusaidia shirika hilo kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi hao.