Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani na Korea kaskazini kukutana inatia moyo-Guterres

Stéphane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa
Picha ya UN/Jean-Marc Ferré
Stéphane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa

Marekani na Korea kaskazini kukutana inatia moyo-Guterres

Amani na Usalama

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Dujarric amesema kuwa Katibu Mkuu Antonio Guterres, ametiwa moyo na tangazo la Marekani na Korea kaskazini kukubali kuzungumza manamo mwezi Mei.

Akizungumza na maripota  mjini New York ljumaa, Dujarric, amesema kuwa Katibu Mkuu atafanya kila awezalo kusaidia kufanikisha mchakato huo na kuongeza kuwa yuko tayari kuitikia mwito wa pande zote husika.

 “ Ameupongeza uongozi wa pande husika na kukariri uungaji wake mkono wa juhudi zote za kuona kama  njia za amani zinafuatwa ili silaha za nuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea kwa kufuata mapendekezo muafaka ya baraza la amani la Umoja wa mataifa”,

Alipoulizwa ikiwa haya ndiyo matunda ya ziara ya hivi majuzi ya Mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa,Jeffery Feltman, nchini Korea kaskazini mwezi Disemba, msemaji wa UN amesema ziara hiyo ilikuwa moja wa kipengele  muhimu cha mustakbala wa mazungumzo hayo.