Miaka 7 ya vita Syria ni fedheha kwa jamii ya kimataifa: UNHCR

9 Machi 2018

Kumbukumbu ya miaka 7 tangu kuanza kwa vita vya Syria machi mwaka 2011, ni fedhea kubwa kwa jamii ya kimataifa, wanasiasa, serikali ya nchini hiyo na wote ambao wamekaa bila kutafuta muafaka wa kukukomesha janga hilo kubwa la kibinadamu, asema  Filipo Grandi, kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbi UNHCR.

Katika ripoti yake, Bwana Grandi amesema zaidi ya watu laki moja wamefariki , milioni 6.5  wamepoteza makazi yao na kutapakaa kila mahali nchini humo, huku zaidi ya milioni tano na nusu wakimbilia nje ya nchi kutafuta hifadhi.

Aidha, Bwana Grandi amesema, UNHCR, na mashirika mengine  ya  kibinadamu wanaendela kufanya jitihada za kutafuta  ufumbuzi kwa waathirika wakuu ndani ya nchi, lakini wanakabiliwa na vipigamizi vya kuwafikia katika maeneo yaliyozingirwa na mapigano.

Msafara wa kibinadamu wa misaada huko  Duma na Ghouta Mashariki tarehe 5 Machi ulikuwa ni hatua ya maendeleo, hata hivyo, makombora yaliyoendelea yalilazimisha malori kuondoka kabla ya nusu ya chakula kutolewa kwa waathirika.

Pia ametoa pongezi kwa  wafadhili kwa  ukarimu, huku akisema kuwa bado misaada yahitajiaka Syria. Mnamo Desemba mwaka jana, mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika mengine 270 walichangisha fedha kiasi cha dola bilioni 4.4 ili kuunga mkono wakimbizi wa nje na dani ya Syria, lakini pengo kati ya mahitaji na rasilimali zilizopo inabaki pana

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter