Zeid aikemea Ufilipino kumuorodheshwa mwanarakati wa haki kama gaidi

9 Machi 2018

Kamishna mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein amekemea  hatua za utawala wa Ufilipino za kumuweka katika orodha ya magaidi, uwakilishi  maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za watu asili, Victoria Tauli-Corpuz.

Bwana Zied amesema  kitendo hicho  hakikubaliki na ni lazima kijibiwe.

(Sauti ya Zeid Ra’ad Al Hussein)

 “Bila shaka hii haiwezi kukubalika dhidi ya  muwakilishi maalum akifanya kazi kwa niaba ya jamii ya kimaaifa kufanyiwa hivyo na ambaye ujuzi wake unahitajika mno na bazala la haki za binadamu.”

Akimnukuu mwakilishi mwenyewe akisem akuwa huenda hatua hiyo imechochewa na uamuzi wake wa kukaripia uawala dhidi ya mauaji ya kiholela kwa wanaodaiwa kuwa wanajihusisha na madawa ya kulevya, vita alivyoanza kiongozi wa sasa wa Ufilipino.

Victoria na wenzake wanalaumiwa kuwa wanachama wa chama cha  Kikomunist cha CCP pamoja na New Peoples Army-NPA.

Pia hivi majuzi imeelezwa  kuwa rais wa sasa wa Ufilipino  alidaiwa kutumia maneno yasiyofaa kumuhusu Muwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa. Hilo nalo kamishna Zeid amelishutumu.

(Sauti ya Zeid Ra’ad Al Hussein)

“Matamshi kama haya kwa kweli hayakubaliki…hayakubaliki.

Ameongeza kuwa kiongozi huyo wa Ufilipino anafaa kuchunguzwa  na wataaalamu wa masuala ya akili.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter