Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati ni huu ni kauli mbiu muafaka- Grandi

Wanawake waliojiandikisha katika elimu ya watu wazima nchini CAR. Picha: MINUSMA

Wakati ni huu ni kauli mbiu muafaka- Grandi

Wanawake

Kauli mbiu ya wakati ni sasa ambayo inaangaziwa leo siku ya wanawake duniani imekuja wakati muafaka, amesema Kamishna Mkuu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR, Filipo Grandi katika ujumbe wake wa siku hii.

Amesema kauli mbiu hiyo inarejelea azma ya UNHCR ya kusaka suluhu na ulinzi  kwa wakimbizi na watu wasio na utaifa bila kujali umri wa mtu, jinsia, rangi au asili yake.

Bwana Grandi amesema lengo lao ni kujenga msingi imara  kufuatia ujuzi, uwezo pamoja na ndoto za wanawake na wasichana  na kuwasaidia kujua uwezo wao kikamilifu.

Amesema wanatekeleza malengo hayo kwa kuwapatia ,wanawake na wasichana, elimu, kazi nzuri pamoja na kupewa huduma sio tu za kiafya bali pia na za kisheria.

Ametoa mfano huko Lebanoni ambako wanawake ni asilimia 50 ya wafanyakazi wa kujitolea wa UNHCR ilhali huko Jamhuri ya Afrika ya Kati UNHCR imejenga vituo vitatu vya kusaidia wanawake kuboresha stadi za kusoma, kushughulikia masuala ya unyanyasaji wa kingono na ghasia za nyumbani.