Ndoa za utotoni za pungua -UNICEF

6 Machi 2018

Idadi ya ndoa za utotoni inazidi kupungua. Hii ni kwa mujibu wa shirika la kuwahudumia watoto UNICEF katika takwimu mpya zilizotolewa leo.

UNICEF imeongeza kuwa mataifa kadhaa yameshuhudia kasi ya ndoa  za utotoni ikipungua na kutoa taswira kuwa kwa ujumla  idadi ya wanawake walioozwa wangali watoto imeshuka kwa asilimia 15 kutoka mtoto 1 kati ya 4 hadi mtoto 1 kati ya 5 katika muongo uliopita.

Akigusia hatua hiyo mshauri mkuu wa jinsia wa UNICEF, Anju Malhotra, amesema wanaoathirika zaidi ni watoto wa Kike akiongeza kuwa “Endapo msichana  akilazimishwa kuolewa angali mtoto, anakabiliwa na athari sio tu za muda mfupi bali na za muda mrefu. Nafasi yake ya kumaliza masomo inapunguka huku nafasi yake kunyanyaswa na mumewe huongezeka, hupata shida wakati wa uja uzito, kuna athari za kijamii na uwezekano wa kuwepo mzunguko wa umaskini”.

Takwim mpya za UNICEF zinaonyesha kuwa idadi ya wasichana walioozwa wakiwa watoto ni takriban  milioni 12 kwa mwaka ikiwa chini kwa kiasi cha ndoa milioni 25 zilizokuwa zinatarajiwa ukilinganisha na kiwango cha miaka 10 iliyopita.

Hata hivyo ili kuweza kukomesha tabia hii ifikapo mwaka 2030, UNICEF inasema juhudizaidi  zinahitajika

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud