Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran iko makini na nyuklia- IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA, Yukiya Amano akihutubia waandishi wa habari Vienna.
Dean Calma/IAEA
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA, Yukiya Amano akihutubia waandishi wa habari Vienna.

Iran iko makini na nyuklia- IAEA

Amani na Usalama

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA, Yukiya Amano amesema serikali ya Iran inatekeleza vilivyo majukumu yake kuhusu nyuklia. 

Bwana Amano amesema hayo leo wakati akihutubia mkutano wa bodi ya magavana wa shirika hilo ukiangazia mpango wa ufuatialiji wa nyuklia nchini Iran, JCPOA.

(Sauti ya Yukiya Amano)

 “Kwa leo naweza kusema kuwa Iran inatekeleza ipasavyo wajibu wake kuhusiana na nyuklia. Ni muhimu sana Iran kuendelea na mkondo wake huo. Endapo JCPOA itashindwa, hiyo itakuwa hasara kubwa ya kuhakiki wa nyuklia”.

Bwana Amano asema wanaendelea kuhakiki vifaa vya nyuklia ambavyo vilitangazwa na Iran chini ya mkataba wa kuvilinda.

Ameongeza kuwa uchunguzi huo unasaidiwa na teknolojia ya kisasa ikiwemo ukusanyaji wa data.

Shirika hilo la nishati ya atomiki limeiomba Iran kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na mipango yake ya kuendeleza nyuklia itakayotumiwa na manowari zake.

Pia amegusia mpango wa nyuklia wa Korea kaskazini akisema kuwa bado ana wasiwasi na mpango huo.

Hivyo ameitaka Korea Kaskazini iheshimu wajibu wake chini ya Umoja wa Mataifa, husususan maamzimio yake na pia kushirikiana vizuri na shirikia hilo.