Tanzania ni mfano wa kuigwa katika amani: Gamba

5 Machi 2018

Umoja wa Mataifa umeipongeza serikali ya Tanzania na jeshi la ulinzi na usalama la nchi hiyo kwa kudumisha amani nyumbani na kwenye operesheni za Umoja wa Mataifa. 

Pongezi hizo zimetolewa Jumatatu na mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye vita vya silaha Bi Virginia Gamba alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya watoto kwenye vijiji vya Shangilitobaya vinavyolindwa na vikosi kutoka Tanzania kupitia mpango wa kulinda amani wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika  Darfur Sudan, UNAMID.

Amesema mafanikio ya vikosi vya Tanzania Darfur ni kielelezo tosha cha kazi nzuri ya jeshi la nchi ndani na nje ya mipaka yake inayotokana na msingi wa amani uliojengeka kwa muda mrefu , jambo ambalo linapaswa kupongezwa

(SAUTI YA VIRGINIA GAMBA)

Bi Gamba pia alipata fursa ya kuzungumza na walinda amani wa Tanzania katika kambi ya Shangilitobaya na kuwahimiza wana nchi wa Sudan kuwasha mwenge wa amani kama uliowashwa na Tanzania juu ya mlima Kilimanjaro

(SAUTI YA VIRGINIA GAMBA )

Walinda amani wa Tanzania darfur ni miongoni mwa kikozi kazi maalumu kilichoundwa kudumisha amani katika eneo la Jeber Marra ambalo kwa muda mrefu lilikuwa halifikiki kutokana na usalama mdogo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter