Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda kuwahakiki wakimbizi-UNHCR

Wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanaosaka hifadhi nchini Uganda. Picha: UNHCR

Uganda kuwahakiki wakimbizi-UNHCR

Amani na Usalama

Uganda imezindua zoezi la kuwatambua  wakimbizi ilionao kwa kuhakiki alama za vidole. 

Zoezi hili imelianzia katika makazi ya wakimbizi ya Oruchinga yaliyoko kusini- magharibi mwa nchi hiyo kuliko na wakimbizi maelfu kadhaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Msemaji wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, Babar Baloch, akizungumza na  waandishi habari mjini Geneva, amesem, lengo la zoezi hili litakalo endelea hadi Septemba mwaka huu wa 2018, ni kuisaidia serikali ya Uganda kurekebisha dosari zozote za takwimu kuhusu wakimbizi.

(SAUTI YA BABAR BALOCH)

“Zoezi la kuthibitisha litahakikisha kuwa wakimbizi na waomba hifadhi  wanaonekana katika mfumo wa kuwasajili na hivyo kuisadia serikali ya Uganda  kuwa na takwimu sahihi. Hii itahakikisha kuwa  vifaa  na huduma zinazotolewa na UNHCR na washirika wake zinawafika walengwa.

Ameongeza kuwa UNHCR ikifanya kazi bega kwa bega na washirika wake,  imeongeza wafanya kazi wengine 400 kuweza kupanua eneo la kufanyia kazi  kwa makazi mengine  zaidi ya 30.

UNHCR imetoa  msaada wa kiufundi kwa zoezi hilo ikiwemo software ya kusajili alama za vidole ambayo tayari imetumika  kuwasajili wakimbizi milioni 4.4 katika nchi 48 duniani.

Pia ameeleza kuwa Uganda ina wakimbizi zaidi ya milioni moja  na inaendeleza mfumo wa kuwakaribisha watu wote ambao wanatoroka mateso na migogoro nchini mwao. Miezi miwili ya mwanzo wa mwaka 2018 , Uganda imepokea wakimbizi wapya zaidi ya 50,000 kutoka mashariki mwa DRC wakitumia mitumbwi kupitia ziwa Albert.