2017 siasa haikuwa na mabadiliko kwa wanawake:IPU

2 Machi 2018

Makwa 2017 kwa ujumla hakukuwa na mafanikio makubwa sana katika ulingo wa siasa  kwa wanawake japo ushiriki wao katika masuala ya uchaguzi uliongezeka kiasi. 

Hayo ni kwa mujibu wa tathimini mpya ya masuala ya kisiasa na nafasi ya wanawake bungeni mwaka 2017 iliyotolewa leo na muungano wa mabunge duniani IPU.

Tathimini hiyo inasema ingawa kulikuwa na idadi kubwa ya wanawake waliogomea uchaguzi mwaka jana na kushinda viti vingi vya bunge kwa asilimia 27.1 ikilinganishwa na alisilimia 22.3 mwaka 2016 , kwa ujumla duniani kote idadi ya wanawake katika mabunge ya taifa imeongezeka kidogo sana asilimi 0.1 toka mwaka 2016  ambapo ilikuwa asilimi 23.3 na sasa ni asilimia 23.4.

Tathimini hiyo iliyotolewa kuelekea siku ya wanawake duniani itakayokuwa Machi 8, IPU inasema katika nchi 20 ambazo wanawake walishinda asilimia 30 ya viti ni kutokana na mpango wa viti maalumu, huku katika nchi 16 ambazo hazina utaratibu huo wanawake walishinda viti asilimia 16.8 pekee.

Martin Chungong ni katibu mkuu wa IPU

(SAUTI YA MARTIN CHUNGONG)

“Ni mwenendo unaotoa hofu kwa sababu inatoa changamoto kubwa katika suala la uhalali wa kuongoza taasisi za serikali , tulichoshuhudia kinahitaji hatua madhubuti zaidi kuchukuliwa na watu wote ikiwemo viongozi wa siasa ili kuongeza idadi ya wanawake bungeni”

Nchi zilizoongoza kwa kuchagua wanawake wengi 2017 ni Senegal asilimia 41.8 , Norway asilimi 41.4, na Kenya ambayo licha ya changamoto idadi ya wanawake ilifikia asilimia kubwa katika historia ya nchi hiyo asilimia 22 kwenye bunge dogo na zaidi ya asilimia 30 kwenye bunge kubwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter