Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walindeni watetezi wa haki za binadamu-UN

Muwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Michael Fost
Picha: MINUSTAH
Muwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Michael Fost

Walindeni watetezi wa haki za binadamu-UN

Haki za binadamu

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu inaonyesha kama watu hao wanaishi na vitisho dhidi yao na hivyo mataifa kushindwa kutekeleza wajibu wake kuhusu suala hili.

Akitoa ripoti hiyo mjini Geneva Uswisi leo, mbele ya baraza la haki za binadamu, muwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya watetezi wa haki za binadamu, Michael Fost, amesema watetezi hao wanakabiliwa na  shida nyingi vikiwemo vitisho, kuzuiwa kutenda kazi zao vilivyo pamoja na kuwabambikizia makosa ya jinai.

Ameongeza kuwa amepokea taarifa nyingi za matumizi ya nguvu za  kupindukia za vyombo vya dola vikitafuta taarifa.

(SAUTI YA MICHAEL FOST)

“madai mbalimbali ya michakato ya kisheria isiyoridhisha,  watu kuswekwa rumande kwa njia zisizofaa au wakati polisi wanapotafuta ushaidi wa mwanzo watu hufanyiwa mambo yasiyohitajika, kama njia ya kupata taarifa kwa nguvu wakiwataka wahusika kukiri makossa kama vile yanayohusika na madawa ya kulevya, ugaidi, pamoja na makossa ya jinai yaliyopangwa.”

Amesema miaka miwili tangu picha  za mwili wa mtoto wa miaka mitatu kutoka Syria aliekuwa anatoroka vita upatikane katika ufukwe wa bahari  nchini Uturuki na kuzusha hisia mbalimbali  duniani kote, leo bado picha kama hizo zinaendelea kuonekana na kutisha hisia za wengi .

Huku maeneo mengi duniani yanakabiliwa na migogoro ya kibinadamu. Watetezi wa haki za binadamu husaidia kuzuia mikasa  kama hiyo kutotokea na pia hulinda  haki za makundi yanayonyanyaswa.