UN haitokata tamaa kamwe Syria:De Mistura

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Steffan de Mistura leo amesema Umoja wa Mataifa asilani hautokata tamaa Syria na utaendelea kusisitiza haja ya usitishaji mapigano kunusuru maisha ya watu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis, De Mistura amesema Umoja wa mataifa utaendelea kupigia debe utekelezaji wa azimio nambari 2401 na kuhakikisha mapigano yamesita kwa siku 30 na pande zote katika mzozo kukomesha uvurumishaji wa makombora ambayo kwa kiasi kikubwa yaakatili maisha ya raia na muhimu zaidi ni kuhakikisha misaada inaruhusiwa kuingia Ghouta Mashariki.
(SAUTI YA DE MISTURA )
“Umoja wa Mataifa hapa haujakata tamaa na hautokata tamaa, hatuna muda na hatutoweza kuwa na raha ya kukata tamaa, hatujachanganyikiwa bali tumejizazatiti kwa sababu vinginevyo hali hii itakuwa Aleppo nyingine.”
Ameongeza kuwa cha msingi hivi sasa ni kukomesha mauaji ya raia. Naye mkuu wa masauala ya kibinadamu Jan Egeland amesema mpango wa Urusi wa kuwa na saa tano za usitishaji vita ni mzuri lakini hautoshelezi kwani
(SAUTI YA JAN EGELAND)
“Ghouta Mashariki ni kitovu cha kutoheshimu sheria za kibinadamu za kimataifa, mashambulizi 24 yameripotiowa kati ya Februari 18-22 pekee, yakijumuisha hospital 14, vituo vitatu vya afya na magari mawili ya kubeba wagonjwa.”
Amesisitiza kuwa hali hii haikubaliki na lazima ikomeshwe.