Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muarobaini wa kupunguza mihadarati ni kutibu waathirika- Ripoti

Dawa za kulevya
UNIS
Dawa za kulevya

Muarobaini wa kupunguza mihadarati ni kutibu waathirika- Ripoti

Afya

Ripoti mpya ya bodi ya kimataifa ya kudhibiti mihadarati, INCB imetaja mambo muhimu ya kuzingatia ili kupunguza matumizi ya madawa hayo duniani.

Ikiwa imefanya tathmini ya mwaka 2017, ripoti inataja mambo hayo kuwa ni matibabu, huduma kwa watumiaji wa mihadarati na programu za kuwajumuisha kwenye jamii zao baada ya kuachana nayo.

Bodi hiyo inataka serikali kwa kuzingatia mambo hayo matatu kutunga sera ambazo kwazo zitashughulikia changamoto zitokanazo na matumizi ya mihadarati.

Changamoto hizo ni pamoja na madhara ya kiafya ya mwili na akili na mtumiaji kupunguza tija na wakati mwingine watumiaji hao kutumbukia kwenye vitendo haramu ikiwemo uhalifu ili kuweza kupata fedha za kununulia mihadarati, lakini pia serikali zimetakiwa kuzingatia haki za binadamu zinapokabiliana na changamoto hizo.

Dr. Cassian Nyandindi anahusika na huduma kwa watumiaji wa mihadarati katika Hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania anaeleza hatua zinazochukuliwa na taifa hilo

(SAUTI YA DR NYANDINDI)

Na wakishajumuishwa kwenye jamii

(SAUTI YA DR NYANDIDI 2)

Mathalani ripoti imetolea mfano kuwepo kwa mfumo utakaowezesha wagonjwa wanaotibiwa na Opiod waendelee na tiba hizo hata wanapoingia kwenye nchi ambako zimepigwa marufuku.