Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati kuhusu utesaji kurejea Rwanda-UN

Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ndogo ya juzuia utesaji ya Umoja wa Mataifa(SPT)
Picha ya UN/ Loey Felipe
Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ndogo ya juzuia utesaji ya Umoja wa Mataifa(SPT)

Kamati kuhusu utesaji kurejea Rwanda-UN

Haki za binadamu

Kamati ndogo ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia  utesaji-SPT-imeamua kurejea Rwanda baada ya kusimamisha uchugunzi huo, Oktoba 2017, ingawa tarehe  ya kurejea huko haijatangazwa.Kamati hiyo pia imesema itazuru Uruguay, Belize na Ureno.

Ziara hizo ziliamuliwa wakati wa kikao cha SPT kilichofanyika mjini Geneva Uswisi. Kamati kuusu utesaji vievile imeamua  kudurusu orodha ya mataifa ambayo hadi sasa yameshindwa kuunda chombo cha kitaifa kinachochunguza uzuiaji katika kipindi cha miaka minne baada ya kuudhinisha.

Kwa sasa orodha hiyo inazijumuisha nchi kama vile :Benini, Bosnia na Herzegovina, Burkina Faso, Burundi, Cambodia, Chile, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon, Liberia,Nauru,Nigeria,Panama, na Ufilipino.

Kamati ndogo ya kuzuia utesaji-SPT inauwezo kufanya ziara yoyote ya kushtukiza kwa eneo lolote ambapo haki za watu zikiwa zinakiukwa katika nchi ambayo iliidhinisha itifaki ya mkataba wa kuzuia utesaji. Vituo hivyo vinaweza kuwa  ni magereza, vituo vya polisi, vituo vya kuwazulilia wahamiaji,  vituo vya kuwashikilia watoto, vifaa vya kudodosa, na hospitali za watu walio na ulemavu wa akili.

"Wakati wa ziara yetu huwa tunasikiliza upande wa serikali na kuishauri jinsi ya kuhakikisha kuwa watu waliokizuizini hawateswi ama kunyanyaswa na pia mahambuzi  kupewa mahali pazuri pa kukaa"amesema Sir Malcolm Evans, mwenyekiti wa SPT, na kuongeza kuwa kila nchi iliyoidhinisha  itifaki hiyo ni sharti kwanza  itilie mkazo wa kuunda mkakati ulio huru na unaotenda kazi zake barabara hatua za kuunda mkamati ya kumaliza utesaji.